News

Posted On: Sep 27, 2026

Kushuka Kwa Ada Ya Ugombea Nafasi Za Ujumbe Wa Baraza La Uongozi

News Images

Chama cha Wahasibu Tanzania (TAA), kinapenda kuwajulisha wanachama wote kuwa, kufuatia maoni yaliyowasilishwa na wanachama kuhusu ukubwa wa ada ya ugombea nafasi za Ujumbe wa Baraza la Uongozi, Baraza la Uongozi limeridhia maoni ya wanachama na ada ya fomu ya ugombea nafasi za Ujumbe wa Baraza la Uongozi imeshuka kutoka TZS 150,000 hadi TZS 50,000 kwa kila mgombea.
Aidha, ili kuwapa fursa wanachama wenye nia ya kugombea nafasi hizo, Kamati imefungua dirisha jipya la uwasilishaji wa fomu, litakalofunga tarehe 6 Oktoba, 2026. Wanachama wote wenye sifa stahiki, kama zilivyoainishwa katika Kanuni za Uchaguzi Mkuu wa TAA, wanakaribishwa kuchukua na kuwasilisha fomu zao ndani ya muda huu.
Fomu zinapatikana katika Sekretarieti ya Chama na kwenye tovuti ya Chama.
Kwa maswali au ufafanuzi zaidi, wasiliana na Sekretarieti ya Chama kupitia simu 0769167278 au barua pepe info@taa.or.tz.
Imetolewa na Kamati ya Uchaguzi ya Chama cha Wahasibu Tanzania (TAA).