Taarifa za uchaguzi mkuu wa Chama cha wahasibu Tanzania 2026
Posted: Sep 26, 2026
FOMUYAWAJUMBEWABARAZALAUONGOZI.pdf
Date: Sep 26, 2026
Chama cha Wahasibu Tanzania (TAA) ni Taasisi iliyosajiliwa mwaka 1983 chini ya Sheria ya Vyama vya Kijamii Sura ya 337 ikiwa na madhumuni ya kuinua, kuilinda na kuisimamia taaluma ya uhasibu Tanzania; na kuhakikisha maadili ya taaluma yanazingatiwa pamoja na ubora wa mafunzo ya taaluma ya uhasibu.
Kamati ya Uchaguzi ya Chama cha Wahasibu Tanzania inapenda kuwatangazia wanachama wake na Umma kwa ujumla kuwa tarehe 17 Oktoba 2026 kutakuwa na Uchaguzi Mkuu wa Chama cha Wahasibu Tanzania kwa nafasi mbalimbali ikiwemo nafasi ya Rais, Makamu wa Rais, na Wajumbe 15 wa Baraza la Uongozi.
Nafasi zote hizi za uongozi ni za kujitolea na si za kiajira wala malipo/mshahara, lengo kuu la nafasi hizi ni kwa ajili ya maendeleo ya Taaluma ya Uhasibu na ya Chama.
Hivyo, Kamati inawaomba wanachama wote wenye sifa stahiki kama zilivyoainishwa kwenye Kanuni za Uchaguzi, na walio tayari kujitolea muda na nguvu zao kwa maendeleo ya Chama, kujitokeza kugombea nafasi hizo.
Fomu za kuomba kuteuliwa zitaanza kutolewa tarehe 26 Septemba, 2026 na mwisho wa kuchukua na kurudisha fomu ni tarehe 2 Oktoba, 2026. Fomu zinapatikana makao makuu ya Chama cha Wahasibu Tanzania na kwenye tovuti ya Chama www.taa.or.tz
Pia, taratibu zote za kugombea zinapatikana katika tovuti ya Chama.
CPA Adv. Emmanuel Laurian Kalibashubao
MWENYEKITI KAMATI YA UCHAGUZI.
