Mkutano Mkuu Wa 43 Mwaka 2026 na Wito Kwa Wanachama Kushiriki Katika Kamati Ya Uchaguzi 2026
Posted: Aug 28, 2026
Date: Aug 28, 2026
Kwa mujibu wa Katiba ya Chama cha Wahasibu Tanzania (TAA), Sehemu ya 11, Ibara ya 3, Rais wa Chama cha Wahasibu Tanzania anapenda kuwajulisha wanachama wote kuwa Mkutano Mkuu wa 43 wa Mwaka (Annual General Meeting – AGM) utafanyika tarehe 17 Oktoba 2026, kuanzia saa 2:30 asubuhi, jijini Dar es Salaam.
USHIRIKI KATIKA MKUTANO
Wanachama wote wanakaribishwa kushiriki katika Mkutano Mkuu huu bila malipo.
Hakutakuwa na ada yoyote itakayolipwa na mwanachama kwa ajili ya kushiriki katika
mkutano huu.
Mkutano Mkuu utakuwa na sehemu kuu mbili. Katika sehemu ya kwanza, ambayo itafanyika asubuhi, wanachama watapata mafunzo maalum kuhusu stadi za kazi na maisha (Soft Skills). Baada ya mafunzo hayo, sehemu ya pili itahusisha mkutano rasmi ambapo wanachama watapata fursa ya kupokea taarifa, kujadili masuala
mbalimbali na kutoa maoni kuhusu maendeleo ya Chama..
