Accountants and Auditors Annual General Meeting

TAARIFA KWA UMMA JUU YA MKUTANO MKUU WA CHAMA CHA WAHASIBU
TANZANIA
Ndugu wanahabari na watanzania kwa ujumla,

Chama cha Wahasibu Tanzania (TAA) kitafanya mkutano wake mkuu wa kawaida wa
37

tarehe 12-13 Novemba 2020 jijini Dar es Salaam kwenye ukumbi wa Kituo cha
Kimataifa cha Mikutano cha Julius Nyerere (JNICC).
Kaulimbiu ya Mkutano Mkuu wa Chama cha Wahasibu Tanzania mwaka 2020 ni:
“Ushiriki wa Wahasibu kwenye Uendelevu wa Uchumi wa Kipato cha Kati
Tanzania: Fursa, Changamoto na Namna ya kusonga mbele” yaani “Accountants’
Participation in Sustainability of Tanzania’s Middle Income Economy:
Opportunities, Challenges and the Way Forward.”

Mgeni rasmi atakuwa ni Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango – Serikali ya
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Baadhi ya ajenda zitakazojadiliwa ni pamoja na:
Ripoti ya Mwaka ya Baraza la Uongozi Taifa; Hesabu zilizokaguliwa za Mwaka wa
Fedha uliopita; Mabadiliko ya Katiba ya Chama cha Wahasibu; na mengineyo.
Mbali ya Mkutano wa Mwaka wa Kikatiba, kusudi lingine la kusanyiko hili ni kujenga
maarifa kwa wahasibu na wakaguzi juu ya umuhimu wao kushiriki katika uendelezaji wa
Uchumi wa Kati wa Tanzania.

 

Kutakuwa na mada muhimu zitakazowasilishwa na wanataaluma ya uhasibu wenye
uzoefu mkubwa kwenye taaluma hii waliolitumikia na wanaoendelea kulitumikia taifa
hili. Miongoni mwa watoa mada ni CPA Ludovick Utouh, Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa
Hesabu za Serikali (CAG) Mstaafu; CPA Pius Maneno, Mkurugenzi Mtendaji wa Bodi ya
Wahasibu na Wakaguzi; CPA Meja Jenerali Mathew Edward Mkingule kutoka Makao
Makuu ya Jeshi la Wananchi wa Tanzania; na wengine wengi.

 

Tukio hili pia litakuwa ni jukwaa la wanataaluma na wadau mbalimbali wa taaluma hii
kuonyesha huduma mbalimbali wanazozitoa kwa kusudi la kubadilishana uzoefu na
kukuza taaluma ya uhasibu nchini.

Gharama za kushiriki mkutano huu wa siku mbili ni shilingi 200,000/= (laki mbili) na
vyeti vitatolewa kwa washiriki pamoja na saa 10 za Elimu Endelevu ya Kitaaluma yaani
10 Continous Professional Development (CPD) Hours.

Tunawaalika wahasibu wote na wahasibu watarajiwa (walio mafunzoni) kushiriki tukio
hili na kushiriki kupata katiba mpya ya chama chao. Tunawakaribisha pia wadau
mbalimbali ambao wako tayari kudhamini maadhimisho haya kwa faida ya umma wa
watanzania wote.

Imetolewa na:

CPA Peter Lucas Mwambuja,
MWENYEKITI,
CHAMA CHA WAHASIBU TANZANIA (TAA)
03 Novemba 2020

 

Download an Attachment

Press Statement AGM 2020